MANCHESTER, ENGLAND
MINO RAIOLA amesema
straika wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic alimtishia kumvunja miguu kama
asingemruhusu Paul Pogba kutua Manchester United.
Wakala Raiola ambaye
anawawakilisha wachdezaji hao wawili sambamba na Henrikh Mkhitaryan alisema
hata hivyo Ibra alizungumza kwa utani.
Wakala huyo
aliandaa mikataba ya nyota wote watatu kutua
United katika usajili wa majira ya jotoin – na Pogba akivunja rekodi ya dunia
kwa kusajiliwa kwa Euro105 milioni.
Pogba na Ibra.
"Zlatan
aliniambia, ‘ukifanya uhamisho wa Pogba sehemu nyingine nitavunja miguu yako',"
alisema Raiola.
Wawili hao wamemfanya
Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho kuwa na uchaguzi mpana wa kupanga
kikosi chake uwanjani, lakini Ibrahimovic amezoea haraka na amewafungia ‘Mashetani
Wekundu’ mabao manne.
Pogba anapaswa
kupambana kuweza kujenga jina Old Trafford.
Hata hivyo Mfaransa
huyo ameonyesha kiwango cha thamani, baada ya kufunga bao katika ushindi wa mabao 4-1dhidi ya mabingwa
watetetezi Leicester City, Jumamosi.
Mourinho.
Kabla ya mchezo huo,
Raiola, alionyesha hisia zake kwamba Kocha Mourinho hamchezeshi Pogba katika
nafasi yake sahihi, ambako ni kushoto kwa washambualiji watatu.
"Pogba bado
anapaswa kutafuta sehemu yake kwenye timu," Raiola alisema. "Napendekeza
nafasi ya kiungo mshambuliaji wa kushoto.
"Kutokana na
nguvu zake, stamina na ufundi... Pogba ataweza kumudu jukumu lake. Lakini Mourinho anatakiwa kufanya uamuzi."
Ibrahimovic.
Nahodha Wayne Rooney akiachwa
benchi dhidi ya Leicester na Pogba akachukua jukumu la kutengeneza mashambulizi,
kiwango kilishoonyeshwa Jumamosi itabaki ni shauri la Mourinho kuendeleza hadi
mwishoni mwa msimu.
Post a Comment