0
LONDON, ENGLAND
LIGI YA MABINGWA Ulaya imerudi tena. Mabingwa wa England, Leicester City baada ya kushinda mechi yake ya kwanza ugenini, Jumanne watakuwa King Power kuwakaribisha mabingwa wa zamani wa michuano hiyo ya Ulaya, FC Porto ya Ureno.
Ni mechi ngumu, lakini itakuwa na kumbukumbu ya staa wao mpya Islam Slimani kukabiliana na timu ambayo alikumbana nayo mara kadhaa alipokuwa Ureno.
Shughuli itakuwa kwa wawakilishi wengine wa England, Tottenham Hotspur ambapo baada ya kuchapwa katika mechi ya kwanza waliocheza nyumbani mbele ya Monaco, safari hii watakuwa ugenini huko Russia kumenyana na CSKA Moscow.

Messi hatakuwapo uwanjani.
Mechi nyingine zitakazopigwa Jumanne ni Monaco dhidi ya Bayer Leverkusen, FC København itakuwa na shughuli mbele ya Wabelgiji Club Brugge, na Wataliano Juventus watakuwa ugenini kucheza na Dinamo Zagreb, wakati shughuli itakuwa huko Ujerumani wakati Borussia Dortmund itakapokuwa mwenyeji wa Real Madrid. 
Mechi hii inasubiriwa kwa hamu kubwa, wakati timu za zamani ya Slimani, Sporting Lisbon itaonyeshana kazi na Legia Warsaw na Sevilla wababe wa Europa League watakuwa na kibarua mbele ya Lyon.   
 Arsene Wenger, kocha wa Arsenal    

Mikikimikiki ya ligi hiyo itaendelea tena Jumatano kwa kushuhudia mechi ya Waingereza watupu, wakati Celtic itakapoikaribisha Manchester City, wakati Borussia M'gladbach itakuwa na kazi mbele ya Barcelona, ambayo haitakuwa na huduma ya staa wake Lionel Messi na Napoli itakipiga na Benfica. 

Ronaldo
Shughuli pevu itakuwa pale Vicente Calderon wakati Atletico Madrid itakapochuana na Bayern Munich, wakati FC Rostov itakipiga na PSV na wababe wa Ufaransa, PSG watakuwa ugenini kwa Ludogorets.
Mechi nyingine ni Besiktas itakipiga na Dynamo Kyiv, wakati Arsenal baada ya kuishushia dozi Chelsea uwanjani Emirates kwenye Ligi Kuu England, itashuka kwenye uwanja wake huo wa nyumbani kuikaribisha FC Basel.


Post a Comment

 
Top