0


MANCHESTER, ENGLAND
ZLATAN IBRAHIMOVIC amedai kati ya timu zilikuwa zikimtolea macho ili atue katika Premier League ni pamoja na Arsenal ya Arsene Wenger.
Straika huyo aliweka wazi kuwa kulikuwa na ofa zilizowekwa juu ya meza kutoka Arsenal na Manchester City kabla ya kufanya uamuzi wa kujiunga na 'Bwana Mipango', Jose Mourinho.

Ibrahimovic
Straika huyo mwenye umri wa miaka 34- alijiunga na Manchester United katika majira haya ya joto pamoja na kwamba amekuwa akiwindwa kwa muda mrefu kutua Premier League.
Ibrahimovic aliweka wazi kwamba kucheza England sio kitu ambacho alikuwa akikihitaji sana hadi kilipofika kipindi cha majira haya ya joto.
Mpaka sasa Ibrahimovic amefunga mabao manne katika michezo minne tangu alipowasili Old Trafford na anajipanga kuanza katika  Manchester ‘derby’ dhidi ya Pep Guardiola wa Man City Jumapili mchana.

Kocha Wenger
Ibra anasema hakuwa na mawazo yoyote ya kutua Arsenal  na City miaka hiyo ya nyuma.
'Nilikuwa karibu kutua Premier League mara mbili – mara ya kwanza Arsenal na baadaye Manchester City,” Ibrahimovic alisema.
“Lakini kamwe haikutokea na sikuhitaji kucheza Premier League,” alisema Ibrahimovic ambaye anajipanga kusomea ukocha  ili akistaafu aweze kukaa katika benchi la Manchester United.

Post a Comment

 
Top