0


LONDON, ENGLAND
DIDIER DROGBA (pichani chini) hawezi tena kuitambia Arsenal uwanjani, lakini anaweza kuitupia maneno katika mitandao ya kijamii kama alivyomtupia Theo Walcott katika Mtandao wa Twitter.
Mambo yote yalianza baada ya winga wa Arsenal, Walcott ambaye ameanza kwa mafanikio msimu huu baada ya kufunga bao la pili na kuiangamiza Chelsea katika ushindi wa mabao 3-0.
Katika kudhihirisha furaha yake baada ya mchezo huo, Walcott alipo-posti picha katika Mtandao wa Twitter akishangilia na kuisindikiza na maelezo ya kufurahia bao alilofunga.

Hata hivyo, Drogba ambaye hakufurahishwa na kiwango cha Chelsea alimpongeza na kasha akamjibu: “Hongera kaka @theowalcott, lakini ni rahisi kwa panya kutamba baada ya paka kuondoka.” 
Enzi zake, Drogba aliinyanyasa Arsenal alipokuwa Stamford Bridge, akifunga mabao15 katika michezo 16 kati ya mwaka 2004 na 2012. 

Walcott akishangilia bao lake.
Kama haitoshi alifunga tena dhidi ya Arsenal katika michezo wa maandalizi ya msimu ilipofanya ziara Marekani, ambako alipopangwa katika kikosi cha kwanza cha wachezaji wa Ligi ya Marekani, MLS All-Stars katika kipigo cha mabao 3-1.
Kabla ya ushindi wa Jumamosi uwanjani Emirates, Arsenal iliifunga Chelesea mara moja katika miaka mitano mwaka 2011- wakati, Cesc Fabregas alipokuwa nahodha wao.

Post a Comment

 
Top