0


MADRID, HISPANIA
CRISTIANO RONALDO wa Real Madrid amefura kwa hasira baada ya kutolewa uwanjani na kocha wake, Zinedine Zidane katika mchezo wa sare dhidi ya Las Palmas.
Ronaldo alishangaa huku akionyesha hasira za wazi alipotolewa katika dakika 72 katika mchezo huo wa Jumamosi usiku– ikiwa ni mara ya kwanza ndani ya miaka saba tangu alipoanza kucheza soka.
Kocha Zidane alimpa mkono Ronaldo wakati akitoka uwanjani, lakini Mreno huyo aliupokea bila ya kukutanisha macho na kocha wake. Moja kwa moja alikwenda kukaa kwenye benchi akiwa amefura kwa hasira.

Ronaldo akikwepa kumwangalia Zidane.
Na uamuzi huo, uliwasha moto baada ya mchezaji wa zamani wa Barcelona B, straika wa Las Palma, Sergio Araujo kusawazisha bao na kufanya matokeo yawe 2-2. 
Hata hivyo, Zidane alitetea uamuzi wake wa kumtoa Ronaldo na kukanusha kwamba straika huyo alichukizwa na kitendo hicho.

 ...akiwa uwanjani.
"Sio kama (Ronaldo) alicheza vibaya," alisema Zidane na kuongeza : " Tunacheza Jumanne na wakati mwingine Cristiano anatakiwa kupumzika. Ilikuwa ni kwa ajili hiyo.  Alicheza vizuri. Usiku nilimwangalia na kufikiria mchezo wa Jumanne.

Ronaldo akitoka...
"Hasira? Hiyo itakuwa ni tafsiri yenu. Kila siku anataka kuwa uwanjani. Huwa tunamtoa wakati mwingine, na tumefanya hivyo leo. Haikubadilisha kitu."

Post a Comment

 
Top