0
Messi
LONDON, ENGLAND
THIERRY HENRY anaamini kujiunga kwa kocha, Pep Guardiola Manchester City kutawavutia wachezaji wenye majina makubwa katika usajili wa mwishoni mwa msimu lakini siyo Lionel Messi.

Henry
Bosi huyo wa Bayern Munich atachukua nafasi ya Manuel Pellegrini mwishoni mwa msimu baada ya kukubali mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya zaidi ya Pauni 15 milioni kwa mwaka.
Na Henry ambaye alifundishwa na Guardiola alipokuwa Barcelona, anatarajia kuwa Man City itakuwa sehemu maarufu zaidi ikiwa chini ya utawala wa Mhispaniola huyo.
“Najaribu kufikiria atawavutia wachezaji wenye majina makubwa kwa sababu ana vyanzo, lakini pia hawezi kuogopa kukuza vipaji.
“Pamoja na kwamba Man City ina academy au vijana wenye vipaji Ulaya ambao hawatakuwa na gharama kubwa, kama tulivyomuona Kingsley Coman, ambaye mpaka sasa yuko Bayern Munich.
“Kama wewe ni shabiki wa Man City, unaweza kuwa na ndoto ya kuwaona baadhi ya wachezaji wenye majina makubwa. Siyo kwa sababu ni klabu kubwa na ina vyanzo, lakini Guardiola ni mtu atakayemvutia mchezaji yeyote duniani.”
Awali Man City ilionyesha kuvutiwa na Messi na kutaka kumpeleka Etihad, lakini Henry hashawishiki kama mchezaji mwenzake huyo wa zamani wa Barca anaweza kujiunga na timu hiyo.
Alipoulizwa kuwa Guardiola anaweza kumshawishi nani kujiunga naye Manchester City, Henry alisema: “ Labda siyo Messi, lakini wachezaji wengi wanataka kufundishwa na kocha huyo."

Guardiola
Pamoja na kwamba klabu iko katika kiwango kizuri, Henry anaamini ubora wa soka utakuwa bora chini ya Guardiola msimu ujao. 
“Pindi Pep akifika Manchester City, atafika na mawazo yake sahihi,' alisema Henry. 
“Naweza kuwahakikishia kuwa timu itacheza soka katika ubora. Atafika na wachezaji wake na wengine atawaondoa. Niamini. Alipokuja Barcelona, aliwaondoa baadhi ya wachezaji. Amefanya hivyo pia Bayern Munich na nadhani atafanya hivyo Manchester City.
“Kuna kitu kimoja unatakiwa kuwa na uhakika nacho – atataka kutawala. Kila wakati atataka  kushirikiana na timu yake katika mabao yatakayofungwa. 
“ Kila siku anataka kuwa mbele, kuwa na mpira, kumiliki kama tunavyojua, na anataka kutawala. Hivyo nawapa hongera, Manchester City.'



Post a Comment

 
Top