0
Gurdiola
MANCHESTER, ENGLAND
PEP GUARDIOLA ameshathibitishwa kuwa ndiye kocha anayefuata klabuni Manchester City na atapewa kitita cha Pauni 80 millioni  kuwasajili Paul Pogba kwa Pauni 50 milioni, Lewandowski kwa Pauni 75 milioni na beki wa Everton, John Stones.
Kocha huyo amekubali dili la kujiunga na Man City la miaka mitatu lenye thamani ya Pauni 15 milioni na kwa wiki atakuwa akichukua Pauni 40,000 zaidi ya kapteni wa Manchester United, Wayne Rooney, mchezaji anayelipwa pesa nyingi katika Ligi Kuu England.
Kocha huyo Mhispaniola atakuwa akipewa nguvu na matajiri wa mafuta na inaonekana kuwa  mchezaji bora wa dunia Lionel Messi anaonekana kuwa mbali na mipangilio yao, Man City inataka kuondoa utamaduni wa wachezaji wakubwa kuhamia Hispania.
Pogba
Guardiola ambaye amewahi kuzifundisha Barcelona na Bayern Munich, amepoteza michezo 19 tu kati ya 239 ya ligi  na Man City kocha huyo mwenye umri wa miaka 45 atawavutia wachezaji wenye majina makubwa. 

Klabu za Chelsea, Barcelona na Real Madrid zitashindana kumwania mchezaji wa zamani wa Manchester United, kiungo  Pogba, 22, ambaye ataondoka Juventus mwishoni mwa msimu na beki Stones, 21.

Lewandowski
Man City ina matumaini kuwa inaweza kuwarubuni wachezaji hao watakuwa chini ya kocha wao huyo mpya.
Mbali na wachezaji hao, Manchester City imejipanga kutoa Pauni 75 milioni kupambana na Real Madrid kumwania straika wa Bayern Munich Robert Lewandowski.
Madrid inaamini itamnasa Lewandowski kwa kuwa alionyesha kuitaka klabu hiyo alipofanya mahojiano na TV ya kwao Poland mapema msimu huu.

Beki wa Everton, Stone (kulia)
Lakini Man City inafahamu kwamba, Guardiola anayemfundisha Lewy katika miaka yake miwili Bayern Munich, anaweza kufanya jitihada kumnchukua straika huyo mwenye umri wa  miaka 27.
Kocha wa sasa wa Man City, Manuel Pellegrini amethibitisha kuwa ataondoka mwishoni mwa msimu kufuatia mkutano alioufanya kabla ya mechi dhidi ya Sunderland Jumanne usiku. 

Post a Comment

 
Top