Pellegrini
MANUEL PELLEGRINI anaangalia uwezekano wa kupata kazi Chelsea baada ya kuendelea kufundisha soka Ligi Kuu England.
Pellegrini ataachana na kibarua chake Manchester City mwishoni mwa msimu na nafasi yake kuchukuliwa na Pep Guardiola.
Na chaguo lake ni kutaka kuendela kufundisha England — na kupata kibarua Chelsea au Manchester United ni moja ya malengo yake.
Wakala wale, Jesus Martinez alisema: “ Ligi Kuu England itabaki kuwa ni ya kusisimua kwake. Ameitumikia kwa miaka mitatu akiwa na Man City na amepagawa kwa ushindani uliopo.
"Atasikiliza ofa na atakazozipata atazijadili na kufanya uamuzi. Mpaka sasa hajapata ofa yoyote mezani. Atakubali changamoto zozote, siyo tu Chelsea, United au klabu kubwa za Ligi Kuu.”
Hiddink
Kocha huyo raia wa Chile ambaye atafikisha umri wa miaka 63 mwaka huu hana mpango wa kuachana na taaluma yake ya ukocha, na pia ameshafungua milango kwa klabu za nyumbani kwao.
Wote Pellegrini na Man City wanatarajia kupata ofa tofauti katika miezi minne iliyobaki msimu huu, na klabu hiyo imeonyesha kutomzuia kufanya mazungumzo na klabu nyingine.
Allegri
Chelsea inaweza kumfukuzia kocha huyo wa zamani wa Real Madrid na hawajamuondoa katika mipango yao ya kumchukua na kuwa wa kudumu mwishoni mwa msimu.
Hata hivyo, nafasi kubwa ya kufundisha Chelsea imetolewa kwa makocha wa Italia, Massimiliano Allegri na Antonio Conte wanaoaminika kuwa wanaweza kuvaa viatu vya Guus Hiddink kama atafeli kuchaguliwa kuwa kocha wa kudumu.
Allegri amemvutia bilionea kwa klabu hiyo, Roman Abramovich tangu alipoanza kuifundisha Juventus miaka miwili iliyopita, wakati Conte atakuwa huru baada ya kuisha kwa mashindano ya Kombe la Ulaya ‘Euro 2016’ akiitumikia Italia.
Conte
Kama sio Ligi Kuu England, Pellegrini anaweza kwenda kufundisha Hispania ambako klabu za Malaga na Villareal zimeonyesha nia ya kumtaka.
Na wakala wake, Martinez amedokeza kwamba anaweza kuvutiwa kuchukua kibarua cha Gary Neville pale Valencia.
Wakala huyo alipohojiwa na Radio ya Hispania alisema: “Pellegrini anaipenda hali ya hewa ya Mestalla.”
Post a Comment