Daniel Sturridge
LIVERPOOL, ENGLAND
DANIEL STURRIDGE yuko tayari
kuondoka Liverpool mwishoni mwa msimu kufuatia
wapinzani wake kuhoji michango wake katika timu hiyo.
Kocha Jurgen Klopp amesema hadharani
kukatishwa kwake tamaa na uwezekano wa Sturridge kuwa fiti na nyota kadhaa wa
zamani wa Anfield wameshauri nafasi ya
straika huyo ipate mtu mwingine.
Suarez alipokuwa Liverpool alikuwa na pacha nzuri na Sturridge
Sturridge amechoshwa na mtazamo huo
na amemuomba meneja wake amtafutie timu nyingine, kwa sababu wapinzani wake
wanaamini hana kiu ya kutimiza majukumu yake katika timu.
Straika huyo mwenye umri wa miaka 26
amebakisha miaka miwili na nusu katika mkataba wake unaompa Pauni 150,000 kwa
wiki, ikimaaanisha Liverpool inaweza kumuuza kwa kiasi kikubwa.
Thamani yake mpaka sasa ni Pauni 60 miliioni lakini rekodi yake ya majeraha inaweza kumshusha hadi kufikia Pauni 20 milioni.
Sturridge bado ana matumaini ya
kurudi katika kiwango kilichomfanya kuwa mmoja wa washambuliaji wa kutisha
Ulaya.
Sturridge akiwasili mazoezini, Ijumaa asubuhi
Anapaswa kuthibisha kupona kwake
kati ya sasa na mwishoni mwa msimu na kutimiza azma ya Liverpool katika
mashindano ya Kombe la FA, Capital One
Cup na ushindi katika Ligi ya Ulaya (Europa
League).
Klabu za Arsenal, Tottenham na Manchester
United zitakuwa sokoni kusaka mastraika wapya mwishoni mwa msimu.
Arsenal ilionyesha nia ya kweli
kumtaka Sturridge Januari 2013, lakini wakati wakijadiliana kuhusu dau lake,
straika huyo akajiunga Liverpool f akitokea Chelsea kwa Pauni 12 milioni.
Sturridge ameumia kila kiungo.
Sturridge anaweza kucheza katika
klabu yoyote ya Ulaya lakini mwenyewe anapendelea kubaki Ligi Kuu England.
Mwaka 2014 aliongoza mashambulizi ya
England katika Kombe la Dunia 2014 na
kocha Roy Hodgson alimsifu kuwa ni straika wa kawaida aliyebarikiwa.
Mwezi Novemba, Klopp alisema: “
Tunatakiwa kukubali kwamba Danny kila mara
amekuwa majeruhi katika miezi ya hivi karibuni, labda miaka.
“Ukiwa na Danny unapaswa kujifunza
aina mpya ya ukali mazoezini na unatakiwa kujifunza kuhusu maumivu makali na
maumivu ya kawaida.”
Wachezaji wa zamani wa Liverpool wakiwemo
Dietmar Hamann na Phil Thompson wameshauri timu hiyo itafute straika mwingine
mpya.
Post a Comment