Ed Woodward
MANCHESTER, ENGLAND
ED WOODWARD Makamu Mwenyekiti wa Manchester
United anatarajiwa kuwekwa kiti moto wiki ijayo katika mjadala wa maendeleo ya
timu hiyo likiwemo suala la kuendelea kwa kibarua cha kocha, Louis Van Gaal.
Makamu Mwenyekiti huyo wa Man United
atatakiwa kuandaa mkutano na wawekezaji Alhamisi kwa njia ya simu kujadili maendeleo
ya robo ya mwisho wa msimu huu.
Kocha Van Gaal amekuwa katika presha
kubwa kutokana na kiwango kibovu na matokeo mabaya kwa timu hiyo ya Old
Trafford ambayo imetolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya mwezi Desemba.
Man united kwa sasa iko katika
nafasi ya nne Ligi Kuu England na nje ya Ligi ya Mabingwa Ulaya japokuwa
Jumanne usiku iliifunga Stoke City mabao 3-0.
Gigs akiwa na Van Gaal
Woodward alipinga alipotakiwa kumpigia
simu ya kumfukuza kazi kocha Van Gaal mwenye miaka 64 lakini presha imekuwa
kubwa kufuatia wapinzani wao, Manchester City kumwajiri kocha, Pep Guardiola ambaye
anatarajiwa kuanza kazi mwishoni mwa msimu huu.
Na Woodward atatakiwa kutoa majibu
juu ya athari za kifedha kwa United kufuatia kushindwa kufuzu mashindano ya
Ulaya kwa mara ya pili ndani ya misimu mitatu.
Pia, inafahamika kwamba Man United imewaandikia
barua mashabiki wake kuwaomba kuwaunga
mkono katika Ligi ya Ulaya (Europa League) watakapopambana na FC Midtjylland baadaye
mwezi huu.
Post a Comment