Chicharito
COLOGNE, UJERUMANI
JAVIER HERNANDEZ ‘Chicharito’ amesisitiza
asingeondoka Manchester United kama Louis van Gaal angemwahidi kucheza lakini
straika huyo amedai hakuwa tayari kukalia benchi.
Chicharito mwenye umri wa maika 27 alijiunga
na Bayer Leverkusen kwa Pauni 7.3 milioni Agosti mwaka jana na amefunga mabao 13 katika michezo 16 ya Ligi ya Bundesliga msimu huu.
Mashabiki waliniambia nibaki
Straika wa kimataifa wa Mexico aliambiwa
na Van Gaal kwamba atakuwa akicheza badala ya Wayne Rooney na hakuwa na chaguo
lingine zaidi ya kuondoka.
“Kama angeniambia miye ni straika namba moja nisiweza kuondoka,”
Hernandez aliliambia Gazeti la The Times. “Lakini nilihitaji kucheza.”
“Nilikuwa kwa ajili ya timu kwa
miaka mitatu. Niliangali jinsi ya kuwa pale, kufanya kazi na kuishi vizuri na
wachezaji wenzangu na nilikuwa tayari. [Ilikuwa ni wakati huo] baadaye nikataka kujiangalia mwenyewe,
kuangalia malengo yangu.
“Mashabiki
walitaka niendelee kubaki lakini nibaki kama mchezaji wa akiba. Sikutaka kubaki
zaidi.
“Nilirahisi kusema hutaki kufanya
mazoezi, kuchati au kuweka picha katika Mtandao wa Instagram kwa sababu huchezi,
huko sasa ni kutaka kugombana na kocha.”
akishangilia bao
Hernandez alisema hana kinyingo na
dhidi ya Van Gaal, kwa sababu alimwambia ukweli.
“Alikuwa ni mkarimu,” straika huyo aliendelea
kusema: “ Kwenye wiki za mwanzo, aliniambia anauona wakati wangu mzuri mbele ya
safari, kwamba nitakuwa na nafasi kubwa ya kucheza kuliko kawaida. Nikajua
nitapata muda wa kucheza.
“Lakini baada ya kuanza kwa msimu, aliniambia
anadhani Wazza atakuwa namba 1wake.”
Hernandez ataiongoza Leverkusen
Jumamosi hii katika mchezo wa Ligi ya Bundesliga dhidi ya Bayern Munich katika
uwanja wa nyumbani.
Post a Comment