Jose Mourinho hakutaka kupewa kazi katikati ya msimu.
LONDON,
ENGLAND
JOSE
MOURINHO ananukia kupata kibarua cha ndoto yake na anatarajia kuwa kocha wa
Manchester United mwishoni mwa msimu.
Imekuwa ni wiki ya kishindo kwa Manchester,
baada ya kutangazwa kwa Pep Guardiola kuwa ataanza kuinoa Man City mwezi wa
Julai, na sasa bila ya shaka watataka
kudumisha upinzani wao kwa Man United
kujipanga kumpa kazi Mourinho.
Upinzani huu unatarajiwa kujirudia England
Hakuna dili lililofanyika mpaka sasa
lakini Mourinho ameupanga moyo wake kuipata kazi hiyo.
Kocha huyo aliyefukuzwa Chelsea
ameweka wazi kwamba anataka kuendelea
kufanya kazi Ligi Kuu England na amekataa ofa mbili za kurudi Hispania
kuifundisha Real Madrid.
Kombe la tatu.
Ofa ya kwanza ilikuwa ni kabla ya Rafa
Benitez kuchaguliwa kuwa kcoha mwishoni mwa msimu uliopita, na nyingine
baada ya kocha huyo kufukuzwa Chelsea in Desemba – kwa hiyo ataendelea kubaki England.
Mourinho alitajwa na Sir Alex
Ferguson mwaka 2013 kwamba angeweza kuwa mrithi wake lakini alikuwa tayari
ameshajifunga kuitumikia Chelsea wakati alipojuwa kuwa anaondoka Bernabeu.
Nafasi hiyo kwa Louis Van Gaal
imekuwa imezidi kuwa ngumu msimu huu, kutokana na Man United ikijitahidi
kupigania kuwepo katika Top Four na wakipanga kufanya mabadiliko mwishoni mwa
msimu.
Akiteta na Ferguson.
Chanzo
cha karibu ya Mourinho kimesema kuwa kocha huyo alikataa kukinoa kikosi hicho
cha Old Trafford katikakati ya msimu, akipendelea zaidi kuanza upya msimu wa 2016/17.
Bosi huyo wa zamani wa Inter Milan na
Real Madrid ameiongoza Chelsea kushinda taji
lake la tatu la Ligi Kuu msimu uliopita, kabla ya kufukuzwa kwa mara ya
pili katika klabu hiyo.
Van Gaal ataaga mwishoni mwa msimu.
Hata hivyo, uvumi uliotawala ni kuwa
machafuko katika kikosi cha Chelsea ulitokana na utata wa sakata la daktari Eva
Carneiro.
Kikosi hicho cha Mourinho kimekuwa
na wakati mgumu kwa kuanza msimu vibaya na kuonekana kupoteza matumaini ya
kutetea ubingwa wao hadi alipofukuzwa Desemba.
Post a Comment