0
Di Maria akifanya vitu vyake PSG.
PARIS, UFARANSA

MCHEZAJI wa zamani wa Manchester United, Angel di Maria amefafanua wakati wake akiwa Old Trafford kama ‘uzoefu wa kusikitisha’ na hataki kuukumbuka.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina alisajiliwa kutoka Real Madrid kwa usajili ambao ulivunja rekodi England wa Pauni 59.7 milioni Agosti 2014.

...akipachika bao
Di Maria alianza kwa nguvu lakini baadaye alipotea vibaya kabla ya kuuzwa  dau linalodaiwa kuwa Pauni 44 milioni kwa mabingwa wa Ligi 1, Paris Saint Germain mwishoni mwa msimu uliopita.
Di Maria alijitahidi kukaa sawa baada ya jaribio la wizi  nyumbani kwake Manchester kabla ya  kuingia katika ugomvi na kocha Louis van Gaal na kukiri kwamba wakati wake akiwa Ligi Kuu haukuwa kama alivyopanga.
Akizungumza na Gazeti la L’ Equipe, Di Maria mwenye umri wa miaka 27 alisema: “Manchester nilipata uzoefu wa kusikitisha sana. Mambo hawakwenda kama nilivyotarajia, nilikata tamaa na sikutarajia. 

...alipojiunga na Man United.
“Kwa kweli,  sikumbuki nini kilitokea na sitaki kukumbuka,”aliongeza.
Baada ya kufunga mabao manne katika michezo 32  akiwa na Man United, Di Maria amerudisha kiwango chake akiwa Paris – kwa kufunga mabao manane na kutoa pasi zilizozaa mabao10 kwa vinara hao wa Ligue 1 ambao wanatarajiwa kukutana na Chelsea katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Pamoja na kiwango kibovi alichoonyesha katika Ligi Kuu England, Di Maria amesisitiza kwamba hana cha kuthibitisha ubora wake dhidi ya Chelsea ili kuifikisha PSG katika fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu huu.



 

Post a Comment

 
Top