0
Neymar
 Neymar mahakamani.
BARCELONA, HISPANIA
STRAIKA wa Barcelona, Neymar ameziweka timu za Ligi Kuu England katika mkao wa taadhari baada ya baba yake, Neymar Snr kudai kwamba straika huyo anaweza kuondoka Barcelona.


Manchester United inaongoza katika mbio za kumwania supastaa huyo wa Kibrazili, sambana na wapinzani wao Man City na Chelsea ambao nazo zinafuatilia hali hiyo kwa karibu.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka Hispania, Neymar Snr, ambaye mwanaye amekutwa na hatia ya rushwa na udanganyifu na Mahakama ya Hispania amwemwambia jaji, klabu ambayo haijatajwa imetoo ofa ya Pauni 144.4 milioni kwa straika huyo.
Wakati akiondoka katika kesi hiyo mjini Madrid, Neymar Snr alisema kiasi hicho kikubwa hakikutolewa na wapinzani wa Barca, Real Madrid.

Kulikuwa na fununu mwezi August, kwamba bosi mmoja wa Man United alikuwa akifanya mazungumzo ya siri kwa ajili ya kumsajili, Neymar mwenye umri wa miaka 23, Old Trafford.
Bosi Louis van Gaal aliwahi kusema kuwa watamsajili mchezaji ‘X ’ kurudisha morali ya mashabiki wa Red Devils fans.
Lakini Man City, ambaye kocha wake, Pep Guardiola ataanza kazi msimu ujao, na Chelsea watakuwa wanakimbia kusaka saini ya Neymar akiondoka Nou Camp.
Neymar, ambaye kesi yake inatokana pindi alipojiunga na Barcelona kutoka Santos mwaka 2013, alisema wiki iliyopita kwamba anapenda kucheza chini ya Guardiola.
Kocha huyo Mhispania anajipanga kuondoka Bayern Munich  na kwenda kumrithi Manuel Pellegrini, Etihad.
Neymar alisema: “Guardiola ni mtu ambaye ninamzimia sana-na ambaye ninapenda kufanya naye kazi.”
Kuna habari kwamba, Neymar hana furaha ndani ya Barcelona na hilo linamfanya kushuka kwa kiwango chake.
Pia, tukio la kukosa penalti katika mchezo dhidi ya Valencia, Jumatano usiku likidaiwa kutokana na kuchanganywa na kesi inayomkabiri.
 

Post a Comment

 
Top