0
Vidal
akiwa Qatar na mashabiki wake.
MUNICH, UJERUMANI

KIUNGO wa Bayern Munich, Arturo Vidal ametishia kuchukua hatua za kisheria Gazeti la Bild la Ujerumani baada ya kuchapisha taarifa kwamba alifika mazoezini akiwa amelewa.

Gazeti hilo liliripoti kwamba Vidal raia wa Chile aliondoka kambini iliyowekwa Qatar katika majira ya baridi na kwenda  kwenye mambo yake binafsi mwezi Januari na alirudi akiwa amekolea kwa kinywaji. 

Lakini Vidal alikanusha madai hayo na kusema ni ya uongo kwa kutumia akaunti yake ya Mtandao wa Instagram.
“Napenda kusema kwamba habari zilizochapishwa leo katika Ujerumani bila shaka si za kweli. Wanasheria wangu tayari wanaandaa madai dhidi ya gazeti na watawajibika kwa kuandika uongo,” aliandika Vidal.

“ Kwa asilimia 100  nilikuwa  karibu na timu yangu na kujiandaa kwa hatua ya kumalizia msimu jambo ambalo ni muhimu kwetu sote.
Gari ya Vidal ilipopata ajali
“Asante kwa klabu yangu kuniunga mkono na asante kwa mashabiki wangu kwa kila siku kuonyesha kwamba wananipenda.”


Mwenyekiti wa Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge alitoa maoni yake: “Tuhuma zote ni uongo mtupu.'' 

Vidal alijiunga na Bayern Munich akitokea Juventus mwishoni mwa msimu uliopita na amefunga mabao matatu katika michezo 28 aliyoitumikia timu yake katika Ligi ya Bundesliga.

Mchezaji huyo mwishoni mwa msimu  uliopita alitengeza vichwa vya habari wakati wa  michuano ya Copa America baada ya kupata ajali ya gari lake aina ya Ferrari.







Post a Comment

 
Top