0


MADRID, HIPSANIA
KOCHA mpya wa Real Madrid, Zinedine Zidane amemfanya Eden Hazard kuwa chaguo lake la kwanza baada ya kupata nafasi ya kuingoza timu hiyo.
Na yuko tayari kumuachia straika, Gareth Bale kurudi katika Ligi Kuu England kwa kutua Manchester United ili kufidia kiasi cha Pauni 100 milioni kumnasa Hazard.

                         Hazard
Zidane  amekuwa shabiki mkubwa wa Hazard na alijaribu kutaka atue Real Madrid kabla ya kufanikisha dili lake la kutua Stamford Bidge kwa Pauni 32 milioni kutoka Lille ya Ufaransa mwaka 2012.
Kama miezi miwili iliyopita Zidane alikiri hadharani kwamba anampenda Hazard pamoja na kwamba alishindwa katika jaribio lake la kumtaka atue Bernabeu.
Bosi huyo sasa yuko katika nafasi ya juu  katika miamba hiyo ya  Hispania, atamwambia rais wa klabu hiyo, Florentino Perez kufanya kila linalowezekana kufanikisha usajili huo.
Zidane akiwa bosi wa  kikosi cha pili cha Real Madrid , Castilla mwezi Novemba alipojitokeza hadharani kumuunga mkono Hazard, alipokuwa akipambana kurudi katika kiwango Stamford Bridge chini ya Jose Mourinho.

Bale
Alisema: “ Sina shaka atarudi katika kiwango chake.Baada ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, Hazard ni chaguo langu.Ni kivutio kumuona akicheza.
“Nitamuona akiitumikia Real Madrid? Nampenda mchezaji huyu, hayo ndiyo ninayoweza kusema.”
Chelsea imemfunga Hazard mwenye ,24, kwa dili la miaka mitano  kwa kumlipa Pauni 200,000 kwa wiki mwishoni mwa msimu uliopita japo kwa sasa uhusiano wake na klabu hiyo siyo mzuri sana.
Kiwango cha Hazard kilishuka akiwa chini ya kocha Jose Mourinho kabla ya kocha huyo hajafukuzwa, na klabu yake iko katika wakati mgumu kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, hivyo itakuwa  vigumu kuigomea Real Madrid.
Mabosi wa Madrid wanajua itawalazimu kutoa ada inayoweza kufikia Pauni100 milioni ili Chelsea kumuachia, lakini wanajiandaa kwa kila kitu kutaka kumchukua mtu wao.
Na sehemu ya dili hilo inaweza kuwa ni kumruhusu Bale kurudi England mwishoni mwa msimu,ambapo Manchester United inaongoza mbio za kuifukuzia saini yake.

Zidane
Chelsea pia watakuwapo sokoni kutaka kumnunua Bale na Manchester City  walionyesha nia hiyo siku za nyuma  lakini Manchester United ndio inayoonyesha kuwa makini kumfuatilia nyota huyo wa zamani wa Tottenham.
Inafahamika kwamba, Bale amekata tamaa baada ya Kocha, Rafael Benitez kufukuzwa Madrid na anangalia uwezekano wa kuondoka Hispania mwishoni mwa msimu baada ya kucheza kwa miaka mitatu.

Post a Comment

 
Top