MADRID,
HIPASNIA
KOCHA
wa Real Madrid, Rafa Benitez amefukuzwa kazi baada ya miezi saba ya kuinoa timu hiyo
na Zinedine Zidane ametangazwa kuchukua nafasi yake.
Wakati
wa kufanya uamuzi ulifika na miamba hiyo ya
Hispania iliitisha kikao cha dharula
baada ya Real Madrid kutoka sare na Valencia Jumapili jioni.
Zidane
Rais
wa Madrid, Florentino Perez alifanya uamuzi huo baada ya timu hiyo kushika
nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi, ikiwa pointi mbili nyuma ya wapinzani
wao, Barcelona na nne kwa vinara, Atletico Madrid.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari Jumatatu baada ya kutangaza uamuzi huo,
Perez alisema: “Bila shaka Rafa Benitez ni mtaalamu na mtu wa ajabu.
Tumeamua kumchagua Zinedine Zidane kuwa kocha mpya wa Real Madrid.”
Zidane na Perez
Akimtambulisha
Zidane, Perez alisema : “ Hii ni klabu yako, huu ni uwanja wako. Na una baraka
zetu zote. Kutoka muda huu wewe ni kocha wa Madrid.
“Najua
neno ‘haiwezekani’ haliishi katika fikra
zako.”
Hata
hivyo, Perez anabaki kuwa shabiki mkubwa wa kocha wa zamani wa Chelsea, Jose
Mourinho.
Akizungumzia
jukumu hilo, Zidane, ambaye alishinda Ligi ya La Liga na Ligi ya Mabingwa wa
Ulaya akiwa mchezaji wa timu hiyo, alisema: “Hii ni klabu nzuri duniani na yenye
ngome ya mashabiki duniani kote. Nataka kuhakikisha kwamba mwishoni mwa msimu klabu
hii itakuwa na kombe.
“Nitafanya
kazi kwa bidii na wachezaji wote na nadhani mambo yatakwenda vizuri. Kesho ndio
kazi itaanza. Nitajitoa kwa moyo wangu wote kwa klabu huu, asanteni.”
Benitez
Michezo
minane ambayo Benitez hajapata ushindi Madrid:
Agosti
23 – Sporting Gijon 0-0 Real Madrid.
Septemba
26 – Real Madrid 0-0 Malaga.
Oktoba
04 – Atletico Madrid 1-1 Real Madrid.
Oktoba
21 – Paris St Germain 0-0 Real Madrid.
Novomba
08 – Sevilla 3-2 Real Madrid.
Novemba
21 – Real Madrid 0-4 Barcelona.
Desemba
13 – Villarreal 1-0 Real Madrid.
Januri
03 – Valencia 2-2 Real Madrid.
Post a Comment