MADRID,
HISPANIA
KOCHA
Rafa Benitez anaweza kufukuzwa baada ya miezi saba ya kuifundisha Real Madrid.
Wakurugenzi
wa klabu hiyo ya Hispania wamekuwa katika kikao cha kumjadili baada ya Madrid
kushindwa kupata ushindi katika mchezo wa Jumapili dhidi ya Valencia.
Rais
wa Madrid, Florentino Perez ameitisha kikao cha bodi Jumatatu mchana ambacho
kitafuatiwa na mkutano wa waandishi wa habari.
Matarajio
ni kwamba Benitez atatimuliwa na mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Zinedine
Zidane atachukua majukumu yake baada ya kuachana na timu B ya Madrid ‘Castilla’
hadi mwishoni mwa msimu.
Rais
Perez anaaminika ni muumini na shabiki
mkubwa wa kocha, Jose Mourinho na kocha huyo wa zamani wa Chelsea anabaki kuwa
chaguo la rais huyo pamoja na kwamba timu kwa sasa atapewa Zidane kwa muda.
Benitez
ameshindwa kupata ushindi katika mechi kubwa katika msimu huu kwa kupoteza pointi
zote mbele ya Villarreal, Sevilla na Barcelona na kuambulia pointi moja moja dhidi ya Atletico
Madrid, Valencia na PSG.
Real
Madrid itafanya mazoezi Jumanne katika viwanja vya Valdebebas ambapo maelfu ya mashabiki watahudhuria kuwashuhudia nyota wa
timu hiyo wakifanya vitu vyao.
Inadaiwa
kuwa, Benitez hajaambiwa au labda anajiandaa na mazoezi hayo lakini kwa kiasi
kikubwa inaaminika Real Madrid sasa itakuwa chini ya Zidane na siyo kocha huyo
wa zamani wa Liverpool.
Baada
ya sare ya Jumapili dhidi ya Valencia, Benitez aliwasili katika chumba cha mkutano Mestalla na
kujaribu kujibu maswali moja baada ya lingine kuhusu hatma yake ndani ya timu
hiyo.
“Ninataka
kuwahakikishia kuwa tutajituma kwa kila mchezo,” alisema.“ Nadhani usiku wa leo
tumefanya juhudi kubwa na ninafarijika na wachezaji.”
Alipoulizwa
kama sare hiyo inaweza kumpotezea kibarua chake, Benitez alijibu: “ Hilo ni kama
tu tunaangalia matokeo. Kiwango kilichooneyeshwa kinastahili zawadi kuliko kupondwa.
“
Siwezi kuwazuia watu kupata hisia kuhusu
kazi yangu. Lakini nataka kuwahakikishia kuwa timu imefanya kazi kubwa sana
leo.”
“Tumeshuhudia
timu kubwa ikiwa na wachezaji 10 waliokuwa wamesimama wakihesabiwa mpaka
mwisho, ingewaje tulikuwa na nafasi kubwa ya kushinda.”
Kapteni
wa Real Madrid, Sergio Ramos alisema alifikiri
bosi wake alikuwa na karata ya ziada kwa ajili ya mechi za raundi ya
pili lakini imekuwa rekodi kwa Real
Madrid dhidi ya timu bora za upinzani ambao umewasaidia wale wote wanaotaka mabadiliko.
Shinikizo la kutimuliwa limemwandama Benitez kwa
wiki kadhaa kutokana na wapinzani wa jadi Atletico Madrid na Barcelona kuwa juu
ya Ligi ya La Liga na mashabiki wa Real Madrid wamekuwa wakipiga kelele za kutaka mabadiliko.
Mashabiki
vichwa ngumu, ambao hawataki kusamehe walionyesha hisia zao mbele ya Benitez
Jumatano iliyopita kwa mara nyingine kwa kumzomea katika mchezo dhidi ya Real
Sociedad.
Hiyo
siyo mara ya kwanza kwa Benetez kuzomewa msimu huu, sauti kama hizo zilisikika
uwanjani baada ya kipigo cha nyumbani
dhidi ya Barcelona.
Kipindi
kifupi cha Benitez, Santiago Bernabeu kimekuwa na ripoti ngumu huku ikiwadiwa kuwa
straika wa timu hiyo, Cristiano Ronaldo na wachezaji wengine wakubwa hawakubaliani na ufundishaji
wake.
Bosi
huyo wa zamani wa Liverpool alipondwa mapema kwa kufundisha soka la kujihami.
Post a Comment