LONDON,
ENGLAND
STRAIKA Wayne
Rooney ameongoza kuwa mfungaji wa kipindi chote wa nchi yake mwaka 2015 na
amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka kwa mwaka wa pili.
Rooney ametangazwa kuwa mchezaji Bora wa Mwaka wa
England kwa mwaka 2015 baada ya kuvunja rekodi ya ufungaji mabao katika timu yake
ya taifa.
Akiwa na umri wa
miaka 30 ameisaidia timu yake kwa kufunga mabao matano
katika michezo minane mwaka huu na kufikisha mabao 50 na kumpita Sir
Bobby Charlton kama mfungaji wa muda
wote.
Pamoja na kwamba msimu huu umekuwa mbaya kwake tofauti na mingine katika timu yake ya Manchester United, kapteni huyo wa timu ya taifa ya England amekuwa sehemu muhimu ya kocha, Roy Hodgson kwa kufanikiwa kufuzu kwa Fainali za Ulaya kwa rekodi ya ushindi kwa asilimia 100.
Rooney amecheza michezo minane kati ya 10 ya England, pamoja na bao lake la penalti dhidi ya Switzerland katika Uwanja wa Wembley mwezi Septemba lilimwezesha kuivuka rekodi ya mwaka 1966 iliyowekwa na mshindi wa Kombe la Dunia, Charton.
Huu ni mwaka wa pili mfululizo Rooney anatajwa kuwa Mchezaji
Bora wa England kati ya mara nne.
Rooney amepata kura asilimia 37 kutoka kwa mashabiki wa klabu za England.Kipa wa timu ya vijana ya Stoke, Jack Butland amechaguliwa kuwa Mchezaji wa Bora wa chini ya umri wa miaka 21 kwa kupaya asilimia 54.
Wachezaji hao watapewa tuzo zao katika mchezo wa England dhidi ya Ujerumani utaopigwa mjini Berlin na dhidi ya Uholanzi utakachezwa Wembley.
Post a Comment