0


MUNICH, UJERUMANI
PEP Guardiola amekiri kwamba amekataa kuongeza mkataba na Bayern Munich kwa sabababu anataka kufundisha Ligi Kuu England.
Bosi huyo wa zamani wa Barcelona ataachana na mabingwa hao wa Ujerumani  mwishoni mwa msimu huu na kujiunga na Manchester City.
Hata hivyo, Guardiola amesisitiza hajafanya uchaguzi wa klabu gani atakwenda kufundisha England.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari,alisema: “ sababu ya kutoongeza mkataba wangu ni nyepesi. Ninataka kufundisha timu ya Primia Ligi.
“Nataka kupata uzoefu wa na kujua hali ya hewa ikoje  na kuangalia mbele. Nina  miaka 44, ni wakati mwafaka wa kwenda kule.
“Kama ningekuwa na miaka 60 au 65 ningekaa tu, lakini nadgni bado kijana zaidi.
“Siaamua ni klabui ipi ninayokwenda kufundisha lakini ninahitaji changamoto mpaya.”
Kocha Carlo Ancelotti ametajwa kurithi kibarua chake Bayern Munich na ataanza kazi mwishoni mwa msimu na kuziacha klabu za England  katika hali ya taadhali.
Kocha wa Manchester City, Manuel Pellegrini anatafutiwa mbadala, wakati Chelsea na Manchester United pia zinatajwa kuangalia makocha wapya.
Lakini kama timu yoyote  ya England itafanikiwa kumnsa Guardiola, kwa maoni yake aliyoyatoa Jumanne  katika mkutano Jumanne yanaonyesha  hatakaa kwa muda mrefu na  alisema hatamchukua mchezaji yeyote kutoka Bayern.
“ Nataka uwanja mpya na kufahamu miji na hoteli,” alisema.

“Miaka mitatu inatosha kwenye timu. Siyo kocha wa kukaa katika klabu kwa miaka 30.” 
Guardiola atawaongoza wachezaji wake wa Bayern Munich kwenda kambini, Doha Jumatano kujiandaa na mchezo wa Bundesliga dhidi Hamburg  Januari 22. 
Pamoja na kwamba kuondoka kwake kunafahamika, Mhispania huyo yuko makini na kazi yake Allianz Arena kwa kuzungumzia tamaa yake ya kushinda michezo ya Ulaya kabla ya kuondoka. 
“Kwa hakika ninahitaji kushinda Ligi ya Mabingwa msimu huu nikiwa na Bayern. Lakini siyo kazi rahisi.

Guardiola alisema amekuwa na furaha na maisha mazuri Bayern  kutoana na uaminifu waliomuonyesha.
" Nadhani Rummenigge hatachukia. Wamefanya kila njia kunibakisha. Siyo sualala fedha ni uamuzi wangu."
Hata hivyo inafahamika kwamba Guardiola anakwenda katika timu ambayo inayofahamika ya Ligi Kuu England  lakini amekuwa akificha.
" Nitakapota klabu ndipo klabu hiyo itaweka wazi," aliongeza. Nina ofa tofauti kutoka England lakini bado sijasaini.
Tangu atue Munich, Guardiola ameshinda mfululizo Kombe la Bundesliga na anaweza kuchukua kwa mara ya tatu msimu huu.
Pia, ameiongoza mara mbili  Barcelona  katika Ligi ya Mabingwa, ameshindwa kutwaa mara ya tatu taji hilo akiwa na Bayern.
Msimu uliopita matarajio yake yalikatishwa na timu yake ya zamani,Barcelona baada ya kuondolewa katika nusu fainali.

Post a Comment

 
Top