0


MANCHESTER, ENGLAND
MANCHESTER UNITED  iko tayari kutoa Pauni 75 milion kumnasa straika wa Real Madrid, Gareth Bale.
Miamba hiyo ya Ligi Kuu Jumatatu ilishuhudia kocha Rafa Benitez akitimuliwa na kuamini kuwa ni ishara ya kutia moyo katika vita yao ya kuvunja rekodi ya kumnasa Bale.
Ingawaje mrithi wa Benitez, Zinadine Zidane amesisitiza hadharani kuwa, straika huyo hauzwi, alikuwa na maisha mazuri chini ya Benitez na amechanganyikiwa kuona anaondoka.
Benitez kocha wa zamani wa Liverpool na Chelsea alijaribu kuitengeneza timu kupitia kwa Bale ambaye alivunja rekodi ya dunia kwa kununuliwa  na Madrid kwa Pauni85 milioni.
Straika huyo alifunga bao lake la nane msimu huu dhidi ya Valencia Jumapili iliyopita.
Manchester United inahitaji  kutengeneza cheche za ubunifu na inataka kumchukua Bale. Straika huyo mwenye umri wa miaka 26, anabaki kuwa chaguo lao namba moja na United inaamini nafasi ya kumnasa imekuwa kubwa zaidi sasa.
Itakuwa mapinduzi makubwa kwa United ikifanikiwa mpango huo na inaamini Bale atakuwa tayari kukubali kurudi katika Ligi Kuu England mwishoni mwa msimu.
Bale

Straika huyo wa zamani wa Tottenham amefanikiwa akiwa na Madrid lakini sasa ataangalia mwelekeo wake baada ya timu kuchukuliwa na Zidane na kuna shaka kama hatakuwa sehemu ya mipango yake.
Rais wa Real Madrid, Florentino Perez amekata tamaa kama Bale atakuwa na mafanikio kama Cristiano Ronaldo kwa kuwa nyota mkubwa katika klabu hiyo.
Lakini Makamu Mwenyekiti wa Manchester United, Ed Woodward anaamini kuchukuliwa kwa Bale kutoka Madrid kutajenga uaminifu Old Trafford.
United inatakiwa kutangaza dau lake linalofikia Pauni 75 milioni ambazo zitaisaidia Real Madrid kujenga kikosi chake.

Post a Comment

 
Top