0


TURIN, ITALIA
 MANCHESTER UNITE KIUNGO wa Ufaransa, Paulo Pogba amesema muda aliokuwa  Manchester United ni sawa na kama alikuwa likizo akilinganisha na kiwango cha juu alichokuwa nacho katika Ligi  ya Serie A na Juventus. 
Pogba aliondoka Old Trafford mwaka  2012 akiwa amecheza katika kikosi cha kwanza mara tatu chini ya Sir Alex Ferguson. 
Mara baada ya kuondoka Ligi Kuu England, Pogba ameisaidia Juventus kwa kuipa mataji mara tatu.  

POGBA
“Watu wanatakiwa kujua kuwa hakuna kitu rahisi Juve,' Pogba aliiambia gazeti la Italia la Stampa. 
“Kuna utamaduni tofauti wa kazi ukilinganisha na sehemu nyingine. Nilikuwa Manchester  na ilionekana kama nilikuwa likizo.
“Hapa tunafanya kazi zaidi. Haya mataji yote hatukuyaiba. Ilikuwa ni kazi mwanzo mwisho.”
Pogba ambaye anahusishwa kuhamia katika timu za Barcelona, Manchester City na Chelsea miezi michache ijayo alipigwa picha akiwa na Mario Balotelli  Jumapili jioni.
Wakala wa Balotelli, Mino Raiola ndiye pia anayemwakilisha Pogba anapanga kufanya mazungumza na Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp kumshawishi kumpa nafasi nyingine Balotelli ndani ya Anfield. 

POGBA alipokuwa Man United.
Akizungumzia tetesi za usajili wake, Pogba alisema yeye si kitu pamoja na kwamba anaangaliwa na timu yenye hadhi  kubwa na inayompa maendeleo. 
“Katika historia jezi ya Juve ni muhimu na nataka kuipa heshima.  Pindi ninapoingalia jezi sioni namba wala jina langu, kitu pekee ninachokiona ni Juve na kuwa na tamaa ya kujitoa kwa asilimia 100 na kushinda,” alisema Pogba. 

POGBA akiwa na Balotelli
“ Mimi siyo kitu kwa kweli, sijafanya kitu katika kazi yangu.”

Post a Comment

 
Top