VALENCIA,
HISPANIA
MCHEZAJI
wa zamani wa Manchester United, Gary Neville amesema anadhani ataendelea kuinoa
Valencia msimu ujao baada ya jana
Jumapili kutoka sare ya mabao 2-2 na Real Madrid.
Neville
ambaye ana mkataba wa miezi sita na timu hiyo, hivi karibuni alikaririwa akisema hatakuwa na muda mrefu katika kufanya
kazi ya ukocha.
Lakini
baada ya sare hiyo na Real Madrid alisema: " Nilikuwa naamanisha kuhusu
miaka 15 hadi 20 nilipozungumzia
kuhusu kendelea na uongozi.
"
Kwa hakika niko hapa kwa miezi sita lakini ninataka kujihakikisha maisha ya
baadaye."
Beki
huyo wa zamani wa Manchester United amevuna pointi tatu katika michezo minne ya Ligi ya La Liga mpaka sasa.
Timu
yake imeizuia Real Madrid ambayo ni moja kati ya timu inayofukuzia ubingwa
ikiwa katika kiwango bora, kwa mchezaji Paco Alcacer kusawazisha bao dakika za
lala salama.
“Jambo
la faraja ni kuiona timu ikiwa fiti, ina
nguvu, inapiga pasi vizuri na tunaokena tuko vizuri katika upande wa beki. Kuna
vitu vinavyofanyika na ninaviamini. Ni kiwango bora mpaka sasa,” alisema Neville.
Post a Comment