0


RIO DE JANEIRO, BRAZIL
RONALDIHHO amekuwa akifanya mawasiliano na klabu kadhaa za Ligi Kuu England ili kujiunga nazo.
Supastaa huyo wa Kibrazili anaamini amebakisha miaka minne ya kucheza na bado anahitajika kila upande wa dunia.
Ronaldinho mwenye umri wa miaka 35 ataiongoza Fluminense katika michezo ya kirafiki  Marekani mwishoni mwa mwezi huu kabla hajamwaga wino kuitumikia timu nyingine katika usajili wa kudumu mwezi huu.

Wakala wale ambaye ni kaka yake Roberto ameweka wazi kwamba kuna timu zinamhitaji straika huyo wa zamani wa Barcelona na PSG zikiweko kutoka nchini mwake.
Alisema : “Nimekuwa nikipokea simu zaidi ya moja kutoka England.
“Ndugu yangu ni mshindani. Anapenda kushinda, kitu hicho watu wengi hawakijui.
“Bado anahitaji kucheza. Hajapata majeraha mabaya sana; mwili wake uko katika hali nzuri.
“Nadhani bado ana miaka mitatu au minne ya kucheza, labda inaweza kuwa zaidi ya hapo.”
Roberto aliongeza: “ Siyo suala la pesa. Anahitaji kucheza. Kitu hicho ndicho ninachomuona kuwa na furaha nacho.”
Haijawekwa wazi ni timu gani zinazomhitaji Ronaldinho lakini inadaiwa ni nusu ya timu zilizopo juu ya msimamo wa wa Ligi Kuu.

Ronaldinho
Kumsajili Ronaldinho kunaweza kuwa ni kwa lengo la dili la kibiashara kama zilivyofanya timu za Mexico, Queretaro na Fluminense ya Brazil ambazo ziliuza jezi na tiketi wakati alipowasil katika klabu hizo.
Kasi ya mchezo katika Ligi Kuu England inaweza kuwa kizingiti  kwa Ronaldinho, hata  hivyo Roberto akiri barani Asia au Amerika kunaweza kuwa hatua nzuri kwa straika huyo.

Post a Comment

 
Top