0


SOUTHAMPTON, ENGLAND
MAISHA ya baadaye ya Straika Sadio Mane ndani Southampton yameingia katika shaka baada ya kuadhibiwa na kocha wake Mholanzi, Ronald Koeman kutokana na kuchelewa kufika katika mkutano wa klabu.
Southampton iko tayari kukubali kumuuza mchezaji huyo Manchester United anayelipwa  kwa Pauni 125,000 kwa wiki kwa dili la miaka mitano.

Ada ya Pauni 30 millioni  itakuwa ya  kushtua kumpeleka Old Trafford ambapo  kocha Louis Van Gaal, anahitaji kuongeza nguvu ya ushambuliaji  kwa kumuonge na Felipe Anderson wa Lazio.
Mane, late for a team meeting ahead of Saints’ 1-0 loss at Norwich yesterday, wants a big move.
Kocha wa Manchester United, Louis Van Gaal kukiri kumfuatilia kwa karibu Msenegali huyo.
Mane alichelewa katika mkutano wa timu kwa saa mbili kabla ya mchezo dhidi ya Norwich na Kocha Koeman alimwadhibu kwa kumuondoa katika kikosi cha kwanza.
Kocha Koeman alishazungumza na Mane kuhusu ukosefu wa umakini katika mazoezi Alhamisi iliyopita na tukio hili la sasa linaashiria kuwa ataondoka Januari.
Bosi huyo wa Southampton hajasema kama atampiga faini mchezaji huyo, lakini amemshutumu kwa kuwaangusha wachezaji wenzake na mashabiki kutokana na kutokuwepo kwake.
“ Tuna vikosi tofauti kwa ajili ya mechi.  Alikuwa mmoja wa wachezaji 11waliotakiwa kuanza, lakini tuna sheria katika timu yetu. Amefanya kosa kubwa sana.
“Simwelewi mchezaji anayekuja akiwa amechelewa kwenye mkutano wa mwisho. Nadhani hakuupokea na kuuzingatia ujumbe wangu wa Alhamisi.’

Koeman alisema: “Klabu inamheshimu kila mmoja, ana majukumu kama mchezaji kwa mashabiki, kwa wenzake, kwa bodi na kwa benchi la ufundi na hii inaumiza sana.”
Hii ni mara ya pili kwa Mane kuadhibiwa  kwa kosa kama hilo. Alifika akiwa amechelewa katika mkutano wa mchezo wa nyumbani dhidi ya Liverpool msimu uliopita.
Kocha huyo alikatishwa tamaa na kitendo hicho ambacho kimetokea siku moja baada ya  Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ralph Krueger kuwatakia wachezaji heri ya mwaka mpya, na kuzumgumzia molari ya timu, nidhamu,  malengo na matarajio.

Post a Comment

 
Top