0


MADRID, HIPSANIA
CRISTIANO Ronaldo amebainisha kwamba hataki kuendelea kuwepo katika soka baada ya kustaafu zaidi ya kuishi kama mfalme

Straika huyo wa Real Madrid, ambaye mwezi ujao atafikisha umri wa miaka 31, anaamini ni vigumu kwake kuachana na mchezo huo ghafla lakini anataka kufurahia maisha na marafiki na familia yake baada ya kustaafu.  
“Kuna maisha mengine badala ya mchezo wa mpira wa miguu,” Ronaldo alisema.

“Nadhani mara ya kwanza itakuwa vigumu, lakini umeniuliza kama nitataka kuwa kocha, naweza kusema hapana. Sitaki kuwa kocha wala rais wa klabu.
“Ukiwa kocha unaweza kusema kuwa una kazi nzuri, pesa, magari, nyumba...lakini hivyo siyo kila kitu. Mfano: Jumamosi moja kutakuwa na pambano la ngumi Las Vegas na nataka kuichukua familia yangu na marafiki kwenda, lakini sitaweza kwa sababu sitakuwa na nafasi. 

“Lakini baada ya kuachana na soka nataka kuishi kama mfalme. Nimekuwa nilivyo leo kwa sababu ya muda nilioutumia bila ya familia yangu na kupitia wakati mgumu.
“Nilikuwa kijana mdogo lakini nililazimika kufanya mambo kama mtu mzima – kujipigia pasi (nguo) mwenyewe. Nguvu ya akili yangu ilianza kutumika wakati huo.”

Ronaldo alipokuwa na Neville, Man United
Ronaldo anajiandaa kwa mchezo wa Madrid dhidi ya Valencia Jumapili hii uwanjani Mestalla. Valencia inafundishwa na  mchezaji mwenzake wa zamani wa Manchester United, Gary Neville.
Madrid kama itashinda mchezo huo itafikisha pointi 39 sawa na Barcelona, baada ya timu hiyo inayofundishwa na Luis Enrique kutoka sare ya 0-0  na Espanyol Jumamosi.


Post a Comment

 
Top