PARIS,
UFARANSA
ZLATAN
IBRAHIMOVIC atakuwa tayari kutua katika Ligi Kuu ya England mwishoni mwa msimu
huu kwa mujibu wa wakala wake.Ibrahimovic, 34, pia amekuwa akihusishwa kujiungana Ligi ya Marekani wakati akitarajiwa kuhitimisha safari yake ya kucheza soka.
Straika huyo wa Paris Saint-Germain atakuwa huru mwishoni mwa msimu na alikuwa haonyeshi ishara ya kuondoka Ufaransa.
Lakini Mino Raiola anapingana na hoja ya mteja wake kucheza soka nje ya England.
Raiola alisema:“Nitapenda kumuona akicheza Ligi Kuu ya England. Nadhani ni mchezo ambao umemfanya kuwa na nguvu, uwezo na ufundi.
“Ni vigumu sasa! Kwa sababu kwa mara ya kwanza anataka kuwa huru , anaweza kuangalia huku na kule na kuwa na mawazo ni kipi anatakiwa kufanya.
“Kuna ofa nyingi sana juu ya meza lakini hajazifanyia uamuzi.”
Raiola aliongeza: “Bila shaka atakuwa na PSG hadi mwishoni mwa msimu.
“Anahitaji kuwa nao na wao wanamhitaji.Tuna uhusiano mzuri sana na klabu hii. Hataondoka Januari.”


Post a Comment