0

SUNDERLAND, ENGLAND
INGEKUWA Bongo wala watu wasingeshangaa. Kingeonekana ni kitendo cha kaiwada tu, lakini kimetokea katika Ligi Kuu England inayoheshimika na wengi.
Kocha wa Aston Villa, Remi Garde amekataa kupeana mikono na mwenzake wa Sunderland, Sam Allardyce kufuatia kipigo cha mabao 3-1 ilichokipata timu yake ugenini.

Kocha Garde kushoto akikataa kusalimana na kocha Sunderland.
Pamoja na kipigo hicho katika Ligi Kuu England, Garde anaweza kukumbana na adhabu kwa kupigwa faini baada ya kukacha kuzungumza muktasari wa mchezo huo kwa waandishi wa habari.
 Kutokana na kipigo hicho wachezaji wa Villa walisumbuliwa na mashabiki wao wakati wakienda kupanda basi nje ya Uwanja wa Light.

Makocha wakizozana
Villa haijapata ushindi katika michezo tisa ikiwa chini ya kocha  Garde na wacheza kamali wa naipa timu hiyo nafasi ndogo ya kufanya vizuri.
Kocha huyo Mfaransa alinaswa akikataa kupeana mkono na mwenzake Allardyce na wakati wa mahojiano ya TV alisema: “Ningefurahi kama kocha Allardyce angekuja mapema kabla ya mchezo na kunisalamia. 

Timbwili likiendelea
“Nadhani ilikuwa ni rahisi kwake kuja baada ya mchezo na kusema ‘hongera’. Lakini katika kuonyesha  ishara ya kukaribisha alitakiwa kuja mapema, lakini sikujali kuhusu jambo hilo. Nilichanganyikiwa na matokeo.”

Kocha Garde
Akiuzungumzia mchezo huo, Garde alisema: “Ni masikitiko makubwa, kama kipigo kingine.  
“Sijakata tamaa, kusema kweli. Ninajaribu kufanya kazi yangu kwa ubora kadiri ninavyoweza kila siku na kila dakika.”

Post a Comment

 
Top