MANCHESTER, ENGLAND
KOCHA Louis van Gaal amemsifu staa wake Wayne
Rooney na kusema kwamba kuanzia sasa mchezaji huyo atakuwa mshambuliaji wake
mkuu katika kikosi kipya cha Manchester United.
Van Gaal pia alimsifia Rooney kwa uwezo wake wa
kukaba akizuia mashambuliaji wa Swansea City kabla ya kufunga bao la ushindi
kwa kisigino. Rooney alihusika pia kwenye bao la Anthony Martial baada ya
kuingia krosi ya Ashley Young na kuwazuga mabeki wa timu pinzani.
Van Gaal alisema: “Siku zote nimekuwa
nikimwambia awe anakimbilia golini, amefanya hivyo na kumpa Martial nafasi ya
kufunga na kisha akafunga bao zuri sana kwa mguu wa kushoto, akifanya hivyo kwa
kisigino. Huwezi kulifikiria bao kama lile kwamba litafungwa.”
Wayne Rooney akifunga bao la ushindi.
Bao hilo la Rooney ni la 238 tangu alipojiunga
na Man United na hivyo kumpiku Denis Law katika orodha ya wafungaji bora wa
muda wote wa timu hiyo. Amebakiza mabao 11 kumfikia 11.
Rooney pia amempiku Andy Cole na kushika nafasi
ya pili kwa ufungaji kwenye Ligi Kuu England baada ya kufikisha mabao 188,
mabao 72 nyuma ya kinara Alan Shearer.
Van Gaal alisema amefurahishwa na Rooney
kutokana na kuonyesha kiwango kizuri katika mechi mbili za karibuni ikiwamo ile
dhidi ya Chelsea.
Kocha huyo raia wa Uholanzi alisema kwamba timu
yake kwa sasa anaitambua kama Man United mpya kutokana na kubadili mfumo wa
kiuchezaji, ambapo sasa atabaki na mabeki watatu tu na wengine wote wanakwenda
mbele kushambulia.
Post a Comment