MANCHESTER, ENGLAND
MANCHESTER
UNITED imeripotiwa kujipanga kumpa kocha wake, Jose Mourinho mkataba wa mpya wa
miaka mitano wenye thamani ya Pauni 65 million, na Mreno huyo yuko tayari
kusaini.
United
imevutiwa na utendaji kazi wa Mourinho Old Trafford tangu alipomrithi Louis van
Gaal Mei 2016 na dili lake jipya litaendelea kumlipa mshahara wa zamani wa Pauni 250,000 kwa wiki ila bonasi zake zitaongezeka mara dufu.
Mourinho,
54, alisaini mkataba wa miaka mitatu na Mashetani Wekundu hao, na atapewa ofa
hiyo baada ya kuwa na mwanzo mzuri
katika msimu wa 2017-18, ambapo kikosi chake kiko nafasi ya pili katika
Ligi Kuu, nyuma ya Manchester City kwa tofauti ya bao moja.
Pia,
Mourinho anavuna matunda yake ya msimu uliopita bada ya kuisaidia Manchester
United kutwaa mataji mawili ya Kombe la EFL na lile la Europa League. Taji la Europa League liiisaidia United kurudi
katika Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na kwamba ilimaliza nafasi ya sita katika
Ligi Kuu.
Kocha
Mourinho amekuwa akipata mafanikio makubwa katika kazi yake lakini ni amekuwa
na sifa ya kukaa kwenye klabu kwa muda mfupi.
Muda
mrefu aliitumia alipojiunga kwa mara ya
kwanza na Chelsea kabla ya kufukuzwa. Alichaguliwa
katika msimu wa 2004-05, na kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu ndani ya miaka mitatu aliyokaa Stamford
Bridge kabla ya kuondoka mapema katika msimu wa 2007-08.
Mourinho
alikaa miaka miwili na nusu na FC Porto na miaka miwili na Inter Milan na
kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na timu hizo.
Misimu
mitatu kabla ya kutimuliwa Real Madrid, alivunja utawala wa wa miaka mitatu ya Barcelona
kutwaa taji la La Liga kwa kuipa timu yake ubingwa wa Hispania msimu wa 2011-12. Kwa
dili hilo jipya la United kuwekwa mezani, Mourinho anajipanga kuwa kocha wa
muda mrefu wa klabu hiyo.
Anaonekana
ameweza kurithi vyema mikoba ya watangulizi wake, David Moyes na Van Gaal na
kuifanya United kuwa na uhai kwa mara nyingine.
Mabosi na mashabiki wa United hawatakuwa
na matatizo na Mourinho Old Trafford kama ataendelea kutwaa mataji, bila shaka na lile taji la
Ligi Kuu.
Post a Comment