PARIS,
UFARANSA
EDINSON
CAVANI (picha chini) na Neymar wameingia katika vita kubwa na kuna ripoti mpya zinazofichua kisa
cha Cavani kumnyang’anya mpira Neymar wakati akitaka kupiga penalti katika
mchezo wa Ligue 1 dhidi ya Lyon.
Wawili hao
walionekana wakizozana kwa muda mrefu wa mchezo huo uliopigwa Jumapili usiku, huku
Cavani akikataa kumwachia majukumu hayo mchezaji mwenzake huyo mpya.
Baada ya mchezo huo, Neymar
na Cavani walikaribia kupigana walipokuwa katika vyumba vya kubadirishia nguo, na
Neymar akamfuta Cavani katika mitandao yake ya kijamii ya Twitter na Instagram.
Kwa mujibu wa Gazeti
la L’Equipe, sababu ya Cavani kutaka kupiga penalti za PSG na kutaka
kuwa Mfungaji Bora wa kikosi hicho na kuvuna bonasi ya Uero1 million.
Inaaminika straika wa
zamani wa PSG, Zlatan Ibrahimovic alikuwa akipata bonasi kwa kuwa alikuwa na
kifungu hicho katika mkataba wake na PSG, ndio maana alikuwa nyuma ya adhabu
zote za mipira iliyokufa za timu hiyo kabla ya kuhamia Manchester United.
Ripoti hiyo
haikuthibitisha kama Neymar ameingia makubaliano kama hayo na PSG au la, lakini
inaaminika kuwa anaweza kuwa nayo.
Kwa sasa Cavani anaongoza
katika chati ya ufungaji ndani ya PSG baada ya kufunga mabao saba katika
michezo sita ya ligi, wakati Neymar akifuatia kwa kuwa na mabao manne katika
michezo mitano hadi sasa.
Post a Comment