MADRID, HISPANIA
DIEGO COSTA anajiandaa kumaliza zama zake klabuni Chelsea na kurudi katika klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid baada ya kwenda kufanyiwa vipimo vya afya mchana wa Alhamisi, Hispania.
Kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone atakuwa amemnasa mtu wake kwa dili lililokubaliwa la Pauni 53 milioni na kumfanya Costa kuweka rekodi ya usajili-mbele ya Radamel Falcao ambaye alisajiliwa kwa Euro 40 milioni kutoka Porto mwaka 2011.
Straika huyo wa kimataifa wa Hispania alikataa kurudi katika viwanja vya mazoezi vya Chelsea vya Cobham katika majira haya ya joto, na kubaki Brazil akiwa na matumaini Atletico Madrid itakubali dili na kumrudisha Madrid.
Hata hivyo, Atletico ilishindwa kuendelea kufuatilia dili hilo hadi siku ya mwisho, inafahamika kuwa Costa hataweza kuitumikia Atletico Madrid hadi Januari kutokana na klabu hiyo kufungiwa kufanya usajili.
Straika huyo mwenye umri wa miaka 28-hajacheza kwa siku 98 tangu alipocheza Hispania katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Macedonia Juni.
Kutokana na dili hilo, inamanisha Costa sasa atarudi Ulaya na kuanza kufanya mazoezi na timu yake na kuungana na wachezaji wenzake kwa maandalizi ya Januari.
Diego Costa akiwa na jezi ya Atletico Madrid.
Post a Comment