0


                     MANCHESTER, ENGLAND
ZLATAN IBRAHIMOVIC ametajwa katika kikosi cha Manchester United kitakachoshiriki Ligi ya Mabingwa wa Ulaya … Habari za uhakika zikidai kwamba yuko katika hatua za mwisho kupona majeraha yake.
Raia huyo wa kimataifa wa Sweden amekuwa nje ya kikosi hicho tangu ya Aprili baada ya kuumia goti katika mchezo wa Europa League dhidi ya Anderlecht.Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 35- alitarajiwa kurudi uwanjani mapema mwakani lakini kupona kwa jeraha lake kwa haraka kumewashangaza hata madaktari wa United.
Habari za sasa zinasema straika huyo mkongwe anatarajiwa kurudi uwanjani dhidi ya Tottenham Oktoba 28. Na anatarajiwa kutoa mchango mkubwa kwa Kocha Jose Mourinho katika mechi za Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi.
 Manchester United itacheza mchezo wa kwanza dhidi ya Basel Septemba 12, lakini Ibrahimovic anaweza kusubiri kucheza mchezo wake wa kwanza katika Ligi ya Mabingwa Ulaya Oktoba 31 pindi Mashetani Wekundu watakapocheza dhidi ya Benfica.
Itakuwa ni hatua kubwa kwa Ibrahimovic ambaye alihofiwa kuvunjika mifupa ya goti. Ibrahimovic ameongeza mkataba wa mwaka mmoja na United mwezi uliopita na utakuwa wa msimu wake wa mwisho katika Ligi Kuu.
Straika kinda James Wilson amepatwa na mshtuko kujumuishwa katika kikosi hicho cha Mourinho cha Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na kwamba hajaitumikia United ndani ya miaka miwili.

Ibrahimovic
Amekuwa akitolewa kwa mkopo katika klabu za Brighton na Derby na amekuwa akisumbuliwa na majeraha.
Kinda mwingine, Marcus Rashford hajaorodheshwa…. lakini mashabiki wa United hawana haja ya kuhofia kwa sababu yuko chini ya umri wa miaka 21 na anaweza kucheza michuano hiyo kwa sheria za Uefa za akitokea katika kikosi cha pili. Mourinho amekuwa akipunguza matarajio ya kurejea kwa Ibra kikosini United kwa kusema: "Lakini sidhani kama kama Zlatan atacheza katika hatua ya makundi. Nina uhakika anaweza kucheza katika hatua ya mtoano lakini kwa hilo, tunatakiwa tuwe tumemaliza katika nafasi mbili za juu.

                                   Ibrahimovic alipoumia goti.
"Simuwazii kabisa na nadhani ni muda mwafaka wa kutolifikiria hilo, mwacheni amalizie matibabu yake, hatua kwa hatua na atarudi pindi akiwa tayari."
Wachezaji walioorodheshwa katika kikosi hicho ni makipa David De Gea na Sergio Romero. Mabeki ni Eric Bailly, Phil Jones, Marcos Rojo, Chris Smalling, Daley Blind, Luke Shaw, Antonio Valencia na Matteo Darmian.

                                  Kinda James Wilson.
Viungo ni Paul Pogba, Juan Mata, Jesse Lingard, Michael Carrick, Ashley Young, Ander Herrera, Henrikh Mkhitaryan, Marouane Fellaini na Nemanja Matic. Mastraika ni Romelu Lukaku, Zlatan Ibrahimovic, Anthony Martial na James Wilson.


Post a Comment

 
Top