PARIS, UFARANSA
NEYMAR ameitaka PSG
kumpiga bei straika mwenzake, Edinson Cavani.
Nyota huyo wa Brazil
anaona haiwezekani kuendelea kuishi na raia huyo wa kimataifa wa Uruguay baada
ya kugombea penalti uwanjani na kufokeana naye katika vyumba vya kubadilishia
nguo baada ya mchezo dhidi ya Lyon Jumapili ambapo PSG ilishinda mabao 2-0.
“Neymar ameshawasilisha
madai yake kwa Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi kwamba hataweza kushirikiana na
Cavani na ametaka straika huyo wa auzwe,” kimesema chanzo ndani ya klabu hiyo.
Mmiliki wa PSG sasa
atakuwa na chaguo la kuamua kutokana na uhusiano huo kati ya nyota wake wawili
ambapo mmoja amevunja rekodi ya usajili ya dunia na mwingine ni nyota wa muda
mrefu kikosini.
Cavani alichukua uamuzi wa kupiga penalti ambayo hata hivyo alikosa lakini Neymar alionekana kuchukizwa kutokana na mchezaji mwenzake huyo kumgomea asipige mkwaju huo.
Cavani alichukua uamuzi wa kupiga penalti ambayo hata hivyo alikosa lakini Neymar alionekana kuchukizwa kutokana na mchezaji mwenzake huyo kumgomea asipige mkwaju huo.
Wawili hao waliendelea
kuonyeshana umwamba hata baada ya filimbi ya mwishona kubidi kutenganishwa na
wachezaji wenzao hali iliyoendelea hadi katika vyumba vya kubadilishia nguo.
Inaaminika kishawishi
kimojawapo cha Neymar kuhamia katika timu hiyo yenye maskani yake katika mji
mkuu wa Ufaransa ni kuwa mchezaji mkubwa baada ya kuishi katika chini ya kivuli
cha Lionel Messi alipokuwa Barcelona.
Na kitendo cha klabu hiyo
kulipa Pauni 198 milioni kwa staa huyo mwenye umri wa miaka 25, kinadhihirisha kuwa
anapaswa kuchukuliwa kama silaha ya maangamizi katika timu.
Kwa upande wake naye,
Cavani amefanikiwa kuwa shabiki wa Kocha, Unai Emery kutokana na kukitumikia
kikosi hicho kwa miaka minne, akitokea Napoli mwaka 2013.
Ikiwa PSG itataka
kumfurahisha supastaa wake mpya itapaswa kumuuza Cavani katika dirsha
linalofuata la uhamisho au kutafuta mwafaka wa wawili hao.
Post a Comment