0
                                               MADRID, HISPANIA
BATA linaendelea, yaani ni Bata batani. Masupastaa, Lionel Messi, Luis Suarez na Cesc Fabregas walichukua warembo wao na kwenda huko Ibiza kuponda raha, katika kipindi hiki wakiwa mapumziko baada ya ligi mbalimbali kumalizika.
Fabregas alikwenda kuungana na marafiki zake hao ambao, kwa sasa bado wanaichezea Barcelona wakati yeye akiwa kwenye kikosi cha Chelsea.
Kiungo Fab alikuwa na kimwana wake, mrembo Daniella Semaan, ambaye hivi karibuni walipata mtoto wao wa tatu, walionekana kuwa wenye furaha walipokutana kwa pamoja Messi na mchumba wake, Antonella Roccuzzo na Suarez akiwa na mkewe, Sofia Balbi.
Wakali hao wote hivi karibuni walikuwa kwenye mechi za kimataifa na waliamua kujipumzisha kwa kuchukua familia zao na kwenda huko bata linakoliwa, Ibiza.
Kwa Messi na Antonella ni kama fungate imekuja mapema baada ya wawili hao kupanga kufunga pingu za maisha mwishoni mwa mwezi huu katika tukio litakalovutia mastaa wengi huko Argentina, ambapo Suarez na Fabregas wanatarajia kuwa wageni waalikwa sambamba na Neymar na Xavi.















Baada ya kutambua marafiki zake wapo huko Ibiza na familia zao, Messi naye aliamua kuchukua familia yake kwenda kujumuika pamoja, kula bata zao.
Kwa pamoja walikodi boti ya kifahari na kuonekana wakifurahia huku Messi, Suarez na Fabregas wakipeana zamu ya kupiga mbizi kwenye maji.
Wakati mastaa hao wa Barcelona wakiponda raha huko Ibiza, mpinzani wao wa karibu kabisa kwenye La Liga, Alvaro Morata wa Real Madrid ameripotiwa kufunga pingu za maisha na kipenzi chake, mrembo Alice Campello huko kwenye mji wa maraha, Venice.
Mastaa wengine wa Real Madrid waliamua kuwabeba jumla warembo wao ni Lucas Vazquez na Mateo Kovacic.

Post a Comment

 
Top