MANCHESTER, ENGLAND
RUUD VAN NISTLEROOY (PIichani chini) kumbe
alionyeshwa mlango wa kutokea Manchester United baada ya kutofautiana na Cristiano Ronaldo mara tu alitoa
maoni yake kufuatia kifo cha baba wa staa huyo wa Ureno.
Awali Mholanzi huyo
alikuwa kipenzi cha Old Trafford, lakini alionyeshwa mlango wa kutokea muda
mfupi baada ya kutaka kushindana na Ronaldo kitendo kilichomfanya Kocha Sir
Alex Ferguson kutokuwa na uamuzi mwingine zaidi ya kumuondoa kikosini.
Sababu ya
kuondolewa kwa Van Nistlerooy imeandikwa katika kitabu kilichochapishwa hivi
karibuni na bosi wa Mawasiliano wa Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony
Blair, Alastair Campbell ambaye ni rafiki wa karibu wa Sir Alex Ferguson.
Kama alivyonukuriwa
na Gazeti la Times, Campbell alionyesha ni kwa kiasi ilikuwa vigumu kumuongoza Van
Nistlerooy kwa kuwa alikuwa mbinafsi, na kumfanya Ferguson kutokuwa na cha
kufanya juu ya mchezaji huyo.
“Ukorofi wa mwisho
aliufanya pale alipomwambia Cristiano Ronaldo amepata baba mpya ambaye ni Carlos
(Queiroz, aliyekuwa kocha msaidizi wa Ferguson) mara baada ya baba wa Ronaldo,
kufafiriki kutokana na unywaji wa pombe,” aliandika Campbell.
“Carlos alimtaka Van Nistlerooy
kuonyesha heshina na akajibu hamuheshimu mtu yeyote pale. Hatimaye aliomba
radhi lakini Ronaldo hakumkubalia.
Ronaldo akiwa na Carlos Queiroz walipokuwa United.
“Alex (Ferguson) alimrudisha
Van Nistlerooy nyumbani pindi aliposikia kuhusu hilo. Lakini hakuwa na uhakika
alichotaka kufanya juu yake,” Campbell aliongeza.
Katika majira ya joto,
Van Nistlerooy alionyeshwa mlango wa kutoka Old Trafford na kuuzwa kwa miamba
ya Hispania, Real Madrid.
Campbell akiwa na Ferguson.
Straika huyo wa Kiholanzi
aliifungia United jumla ya mabao 95 katika
Ligi Kuu England katika michezo 150 aliyocheza.
Post a Comment