BARCELONA, HISPANIA
CRISTIANO RONALDO amerudi uwanjani Alhamisi kuitumikia Real
Madrid katika Ligi ya La LIga na kukaribishwa na kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Real Betis.
Kwa upande wa pili, hasimu wake mkubwa staa wa Barcelona, Lionel Messi ambaye msimu
uliopita aliondoka mikono mitupu huku Ronaldo akiweka rekodi zake kibao katika
soka sasa anatesa.
Msimu huu Messi hataki kuchezewa kabisa ambapo, licha ya
Barcelona kuonekana kuyumba amehakikisha inakamata usukani wa La Liga ikiwa na
pointi 15 ikishinda mechi zake zote tano.
Lakini, achana na hizo pointi 15 za Barcelona, ishu kubwa ni
kuwa Messi ameanza kutupia nyavuni kwa kasi msimu huu, ambapo mpaka sasa ana
mabao tisa huku Ronaldo akiendelea akirudi katika mechi ya kichapo baada ya
kutumikia adhabu ya kukosa mechi tano.
Pia, Messi ameweka rekodi yake nyingine kwenye kikosi cha Barcelona
akifunga bao la 300 katika Uwanja wa Camp Nou.
Messi ameweka rekodi yake hiyo tamu kwenye mchezo dhidi ya
Eibar, ambapo alifunga mabao manne wakati Barcelona ikiondoka na ushindi wa
mabao 6-1 kwenye ushindi wa mechi sita mfululizo.
Messi akishangilia bao lake...
Kwa mabao hayo manne, Messi amefikisha mabao tisa msimu huu
kwenye La Liga hivyo, kumfanya Ronaldo ambaye kikosi chake cha Real Madrid kiko
nafasi ya tano na pointi nane akiwa na mlima mrefu wa kupanda.
Kwa mabao hayo dhidi ya Eibar, kunamfanya Messi kupiga hat-trick
ya pili kwa msimu huu, ambapo ya kwanza alifunga katika mchezo dhidi ya
Espanyol wakati Barcelona ikishinda 5-0.
Ronaldo mikono kichwani.
Katika mchezo huo, Messi alianza kupachika bao la kwanza kwa
mkwaju wa penalti dakika 20 tu, akipiga kwa ufundi kabisa.
Ronaldo akipambana dhidi ya Real Betis.
Mabao mengine yalifungwa na Denis Suarez, Paulinho ambaye ni bao
lake la pili tangu asajiliwe na Barcelona kutoka Ligi Kuu ya China.
Post a Comment