0
MANCHESTER, ENGLAND
KEVIN De Bruyne, kiungo wa Manchester City amempa pigo Kocha Pep Guardiola baada ya kuripotiwa kuumia nyama za paja na anaweza kuwa nje kwa wiki nne.
De Bruyne aliumia katika mchezo wa ushindi wa mabao 3-1n katika Ligi Kuu England Jumamosi dhidi ya Swansea City.
Kiungo huyo alitolewa katika dakika ya 81 akihisiwa kubanwa na misuli na mbelgiji huyo alisema atakuwa nje kwa mwezi mmoja kutokana na tatizo hilo.

De Bruyne akiwa kazini.
Hiyo inamaan De Bruyne ataukosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Celtic Jumatano na michezo ya Ligi Kuu dhidi ya Tottenham na Everton, wakati kukiwa na wasiwasi mkubwa wa kuikosa safari ya Barcelona Oktoba. 19.
Pia, De Bruyne atakosa mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia kati ya Ubelgiji na Bosnia-Herzegovina na Gibraltar Oktoba. 7 na 10.
Hata hivyo, imeripotiwa kwamba City itatoa taarifa kamili kuhusu majeraha ya De Bruyne Jumanne.

aliwahi kuumia hivi siku za nyuma.
Akizungumza baada ya mchezo huo wa Jumamosi, bosi wa City, Pep Guardiola alisema: " Ninadhani amejeruhiwa.


... akiwa katika majonzi baada yakutoka uwanjani.
"Usiku huu tunarudi Manchester, kesho ataonwa na madaktari. Ni jambo la kusikitisha. Ni muhimu kwetu. Kwa jinsi alivyokuwa akihisi ilionekana kama ni misuli lakini mimi siyo daktari."

Post a Comment

 
Top