LONDON, ENGLAND
ARSENE WENGER amemsifu mabadiliko na
uwezo wa Theo Walcott uwanjani na anaamini Arsenal itanufaika na uchezaji wake
msimu huu.
Walcott mwenye umri
wa miaka 27, alifunga Jumamosi bao lake la
tatu katika michezo sita ya Ligi Kuu
msimu huu- wakati The Gunners ilipoibamiza Chelsea mabao 3-0 na kuweka rekodi
ya ushindi kwa mara ya kwanza dhidi wapinzani wao hao wa London, tangu 2011.
Walcott, mchezaji wa
kimataifa wa England hatarajiwi kurudia kitendo cha kukatisha tamaa cha msimu
wa 2015-16, na mar aka mara kujikutana katika benchi la Arsenal na kukosekana
katika michuano ya Euro 2016.
Walcott akikimbiza
Lakini Wenger anahisi
anapaswa kumpa moyo ili aweze kuwa mchezaji wenye ushindani zaidi.
"Ameiva,"
Wenger alikaririwa "Pindi mchezaji anapopambana na aina hii ya ukatishwaji
tamaa kwa kile alichoahidi akiwa na umri wa miaka16 (alipoanza kwa mara ya
kwanza kuingia uwanjani), jinsi alivyokabiliana na hali halisi kila siku nahisi
kuna kitu cha ziada kwa kijana huyu.
"Ni mjanja,
Theo. Anatahimini vizuri kiwango chake. Ana umri wa miaka 27, ni umri muhimu.
Walcott na wenzake wakishangilia bao.
"Anatumia asilimia 90 kushambulia
na asilimia10 kulinda. Leo hii kazi yake ni 50-50. Anafanya kazi katika njia
zote na anafanya kwa majukumu."Daina siku zote niliona kuna akili na maarifa kwa kijana huyu. Ni kijana mwenye kutathimini kiwango chake na ubora. Nilisema wakati tunaanza msimu kwamba tutamuona Theo Walcott tofauti. Ninaweza kuona amefanya uamuzi na kubaki hapo."
Walcott alikatishwa tamaa katika anga za kimaitafa na Wenger amekiri kwamba wamepoteza thamani ya mchezaji huyo.
Wenger
"Lilikuwa pigo kubwa kwake
kutokwenda Euro (katika majira ya joto)," Wenger alisema. "Alikwenda
katika mashindano ya Kombe la Dunia 2006 (na hakucheza). Hakuchaguliwa mwaka 2010
(na alikuwa majeruhi 2014). Sasa tuko 2016 na hatakwenda katika mashindano ya
Kombe la Dunia yanayofuata."
Post a Comment