MADRID, HISPANIA
IMEBAINIKA, kumbe kocha wa zamani wa
Chelsea, Mreno Jose Mourinho amekataa kazi ya kuinoa Real Madrid kwa sababu
bado ana ndoto za kuifundisha Manchester United.
Mourinho
alipelekewa ofa hiyo kabla ya kupewa, Zinadine Zidane lakini aliikataa kwa sababau
anataka kubaki Ligi Kuu England na
kuchukua nafasi ya Louis van Gaal.
Real
Madrid alizungumza na Mourinho katika
msimu wa sikukuu ili achukue nafasi ya Rafa Benitez.Mabosi wa Madrid walitaka kumpa kazi Mourinho kwa sababu awali Zidane alionyesha wasiwasi wa kukubali jukumu hilo.
Inafahamika kuwa, Rais wa Madrid, Florentino Perez ni shabiki mkubwa wa Mourinho na alitaka kujua kama bosi huyo wa zamani wa Chelsea atakubali kibarua hicho.
Lakini Mourinho ameitosa ofa hiyo ya kurejea Bernabeu baada ya kuondoka miaka mitatu iliyopita.
Mourinho
Mreno
huyo amekataa kazi hiyo kwa sababu ya siasa za klabu hiyo na tabia ya Perez ya
kukubali ushauri wa kuwafukuza makocha
haraka.Lakini sababu kubwa ya kupigia mstari ni kwamba Mourinho bado anataka kubaki England ndio maana ameendelea kuishi London tangu alipotimuliwa Chelsea mwezi uliopita.
Tatizo la Mourinho hana sapoti ndani ya utawala wa Old Trafford na kama Louis Van Gaal atafukuzwa mbadala wake anaweza kuwa Ryan Giggs ambaye anakubalika sana na uongozi.
Man United inaonekana inataka kubaki na Van Gaal lakini wakati Mourinho akiwa bado yuko sokoni, lazima shinikizo litakuwa linamuandama Mholanzi huyo.
Mourinho anaweza kufanikiwa kupata kazi hiyo ya kuinoa United lakini anaweza kupoteza muda na ni bora angeangalia kazi nyingine zinazokuja.
Zidane anaonekana kama chaguo la kucheza kamari kwa sababu ya kukosa uzoefu wa kazi hiyo.
Rais wa zamani wa Real Madrid, Ramon Calderon pia alisisitiza Mourinho alikuwa chaguo la kwanza kabla ya Zidane na alipita kwa kura nyingi.
Calderon alisema: " Aliyechaguliwa alikuwa ni Mourinho, lakini ameamua kutokuja kwa sasa.
"Zidane amekuwa kocha kwa kuwa alikuwapo pale. Nina uhakika walimtaka Mourinho.
Kocha Mourinho
"Wanadhani
wanacheza bahati nasibu kumpa nafasi Zidane. Nadhani anaweza kuwa kocha mzuri
kama alivyokuwa mchezaji, kwa sababu
amekuwa kocha wa timu ya vijana kwa mwaka mmoja na nusu, na kabla ya hapo alikuwa ni msaidizi wa Carlo Ancelotti- huo
ni uzoefu tosha.”"Ni kama ilivyo kwa Gary Neville kwa Valencia, lakini jambo moja gumu ni kwa sababu Real Madrid siyo Valencia.”
Pia, Calderon anaamini kwamba Benitez amefukuzwa Real Madrid sasa kwa sababu ya kukwepa kumlipa mshahara wa miaka miwili.
" Walipaswa kumfukuza sasa kwa sababu kabla ya Januari 15 wanapaswa kumlipa mshahara wa mwezi mmoja.
"Baada ya hapo, ingekuwa ni mishahara miwili. Huo ndio ukweli wa kufanya uamuzi huo sasa," alisema Calderon.
Post a Comment