0


STOKE, ENGLAND
 JORDAN Ibe ameifungia Livapool bao la pekee katika mchezo wa fainal ya kwanza ya Kombe la Capital One jana Jumanne dhidi ya Stoke lakini wachezaji wa timu hiyo wamelala na viatu.
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp  aliingiwa na wasiwasi baada ya wachezaji wake watatu kuumia nyama za nyuma ya paja  katika Uwanja wa Britannia.

Kiungo Coutinho akiugulia maumivu
Philippe Coutinho na Dejan Lovren walilazimika kutoka  katika kipindi cha kwanza wakati  beki Kolo Toure alicheza baada ya kufungwa bandeji katika dakika za lala salama.
Coutinho alilazimika kutoka dakika ya 18 na nafasi yake kuchukuliwa na mfunguji wa bao hilo, Ibe.

Beki Lovren akiugulia
Kocha Klopp alichanganyikiwa zaidi  baada ya beki wake Lovren kuumia  katika kipindi hicho cha kwanza. 
Toure alionekana kuwa mchezaji wa tatu kupatwa na majeraha hayo  lakini Mu-ivory Coast huyo alicheza akiwa na maumivu katika dakikia hizo za majeruhi.
Coutinho na Lovren ambaye nafasi yake ilichukuliwa na James  Milner katika dakika ya 34, watakuwa nje kwa kipindi kirefu cha matibabu wakati timu yao ikiwa inakabiliwa na michezo migumu ya Ligi Kuu dhidi ya Arsenal na Manchester United hivi karibuni.

Beki Kolo Toure naye akiugulia maumivu
Wachezaji hao wamejiunga na Daniel Strirridge (anadaiwa atarudi hivi karibuni), Jordan Henderson, Martin Skrtel.
wengine ni Joe Gomez (goti), Jon Flanagan (goti), Mamadou Sakho (goti), , Jordan Henderson (kisigino), Jordan Rossiter (misuli ya paja), Danny Ings (goti), na Divock Origi (misuli ya paja).

Post a Comment

 
Top